Wabunge wamepiga Kura na Kumchagua tena Waziri Mkuu, Shigeru Ishiba kuendelea na nafasi hiyo licha ya Muungano wake kupoteza wingi wa Wabunge katika Uchaguzi wa Baraza la chini Mwezi uliopita.
Ishiba ameshinda kwa Kura 221 dhidi ya Kura 160 za Yoshihiko ikiwa ni marudio ya Uchaguzi ya Kihistoria ambayo hayajashuhudiwa Nchini humo kwa takriban Miaka 30.
Imeelezwa kuwa kufanya vibaya kwa Chama cha LDP kunatokana na Kashfa za Rushwa ambazo zilimlazimu Waziri Mkuu aliyepita, Fumio Kishida, kutakiwa kuomba radhi Bungeni Januari 2024.