Russia inafikiria kuanzisha “wizara ya ngono” kama njia ya kushughulikia tatizo la kupungua kwa idadi ya watu kuzaliwa nchini humo.
Nina Ostanina, mwenye umri wa miaka 68 na mtu anayeaminiwa na Rais Vladimir Putin, anayeongoza Kamati ya Ulinzi wa Familia katika Bunge la Russia, anapitia ombi linalotaka wizara hii ianzishwe.
Hatua hii ni moja ya juhudi zinazofanywa na serikali za kukabiliana na hali ya kupungua kwa idadi ya watu nchini Russia, hali ambayo imezidi kuwa mbaya kutokana na vita inayoendelea nchini Ukraine.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, wazo hili linakuja wakati ambapo viongozi wa Russia wanajaribu kuongeza kiwango cha uzazi ili kukidhi wito wa Putin wa kupambana na mzozo wa idadi ya watu.