Timu ya Nigeria yadai ilitelekezwa Airport,yagomea mechi ya Libya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: timu-nigeria-yadai-ilitelekezwa-airportyagomea-mechi-libya-104-rickmedia

Timu ya Taifa ya Nigeria ilitarajiwa kutua Jijini Benghazi, jana Oktoba 14, 2024 lakini Ndege yao ikaeleka Mji mwingine wa Al Abraq, uliopo Kilometa 230 kutoka Benghazi, ambapo inadaiwa hakukuwa na Maafisa wa Libya walioenda kuwapokea.

Afisa wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), Promise Efoghe, amesema hawakujulishwa sababu ya mabadiliko ya Ndege, “Walitufungia ndani ya Uwanja wa Ndege usiku wote, ni kama tulikuwa jela.”

Straika wa Nigeria, Victor Boniface, amesema walitelekezwa bila kuwa na Chakula, Wi-Fi wala Huduma ya kulala. Wakati huohuo Shirikisho la Soka la Libya (LFF) limekanusha kuhusika na kilichotokea na kusema mabadiliko ya ratiba ya Ndege sio jukumu lao.