Ubomoaji wa nyumba eneo la Jangwani Jijini Dar Es Saalam kuanza April 15,2024

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: ubomoaji-nyumba-eneo-jangwani-jijini-dar-saalam-kuanza-april-152024-213-rickmedia

Serikali imesema Mradi wa Bonde la Msimbazi utaanza Aprili 15, 2024 ambapo utaanza kwa Ubomoaji wa Nyumba katika eneo la Jangwani zilizopo kando ya Mto Msimbazi.

Mradi huo utasimamiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) ambapo taarifa imeeleza hadi kufikia Februari 29, 2024 ilikuwa imelipa Fidia ya Tsh. Bilioni 52.61 kwa wamiliki wa nyumba 2,155 kati ya 2,329.

Mradi huo unatarajiwa kuchukua Miaka 5 na utagharimu Dola za Marekani Milioni 260 (Tsh. Bilioni 675) kwa kujenga Karakana mpya ya Mabasi ya Mwendokasi eneo la Ubungo Maziwa na Miundombinu ya Kuzuia Mafuriko.

Aidha, Fedha hizo zitajenga Daraja la Jangwani, Bustani ya Jiji, Uendelezaji wa Maeneo ya Makazi na Biashara, Kupanua Mto Msimbazi, Kuongeza Kina na Usimamizi wa Taka Ngumu.