Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika majimbo mawili muhimu ya North Carolina na Georgia, hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi.
Hadi sasa, Trump amepata kura za majimbo (electoral college) 248 huku mpinzani wake, Kamala Harris akipata kura 214. Ili kutangazwa mshindi, lazima mgombea apate kura 270 za majimbo, hivyo Trump ameikaribia nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Rais huyo wa zamani, anaongoza kwa kura 67,341,630 (sawa na asilimia 51.2), wakati Kamala akiwa na kura 62,080,264 (sawa na asilimia 47.4) ya kura zilizohesabiwa hadi sasa.