Klabu ya Arsenal imemuuza Midfielder wao Granit Xhaka kwa klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen kwa dau la Euro Milioni 21.4. Xhaka amesaini mkataba wa miaka mitano ya kuitumikia klabu hiyo ya Ujerumani
Xhaka alijiunga na Arsenal mwaka 2016 na alitarajiwa kumalizana na washika mitutu hao mwaka kesho 2024. Xhaka amesginda magoli 23 ndani ya klabu ya Arsenal kwenye michezo 297 aliyocheza na kuiwezesha klabu hiyo kushinda mataji mawili ya FA na kuiwezesha klabu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye msimu uliopita.
Mwaka 2021 Arsenal walikataa dau la Euro 12.9 kutoka kwa klabu ya Roma na mwaka uliofuata walimuongezea mkataba ambao ungeisha mwaka 2024