Staa wa Muziki #Harmonize ambae hapo mwanzo alitangaza kuwa atachukua Fomu kwa ajili ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Tandahimba, Mtwara Amesema kuwa kutokana na Sheria za Chama cha #CCM na Bunge hajioni kama mtu mwenye vigezo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika..
"Nimepitia Sheria za Kamati Yaa Maadili Ya Chama & Bunge
Simuoni KONDEBOY Kwaninavyoona Hata Kusema
BOMBOCLAAAATY Sitoruhusiwa 😂 Niwapongeze wana @ccmtanzania mliojitoa Kutangaza Nia ZaKugombea Nafasi Tofauti Tofauti Especially Vijanaa 👏 DINI YENYE WAFUASI WENGI UJUE INAKUBALIKA !!! Tandahimba Chaguani Kiongozi Bora Atake Msaidia RAIS wetu miaka 5️⃣ Ijayo!!!!!!! am Hungry for the Grammy & More Success Music"