Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani imewapiga marufuku wasanii wa muziki wa #RapPunk kutoka Uingereza kwenda kutumbuiza Marekani baada ya kuonekana kuwaongoza mashabiki katika kuimba kauli za kuunga mkono wakazi wa Gaza walioko katika hali ya mashambulizi na kutakia kifo majeshi ya Israeli, maafisa walisema Jumatatu.
Viza za #BobVylan na kundi lake zilizuiliwa kutokana na hotuba yao ya chuki waliyoitoa Glastonbury, ikiwemo kuwaongoza mashabiki katika kauli za kutakia watu kifo, alisema Naibu Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje #ChristopherLandau katika taarifa.
Rapa huyo aliongoza hadhira ya Tamasha la Glastonbury Jumamosi katika kuimba kauli za "free, free Palestine" na "death, death to the IDF" (Jeshi la Ulinzi la Israeli), kulingana na video zilizoonekana mitandaoni mitandaoni.
Baadhi ya wanaharakati wa upande wa Palestina wanasema ni wito wa amani katika eneo hilo. Wengine wanadai kuwa maneno hayo ni ya chuki.
Afisa mpelelezi wa Polisi wa Somerset amepewa jukumu la kuchunguza kama kuna sheria yoyote ya uhalifu wa chuki iliyovunjwa wakati wa maonyesho hayo, maafisa walisema Jumatatu.
Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia iliwalaani wasanii hao, ikiwatuhumu kwa kuchochea chuki.