Aliemfungua mashtaka dhidi ya Staa wa Muziki #ChrisBrown ameripotiwa kuwasilisha ombi la kufuta kesi ya madai iliyotokana na kisa cha ugomvi wa usiku iliodaiwa kutokea kwenye Club ya usiku lakini mashtaka ya jinai dhidi ya #Chris bado yanaweza kuwa yanaendelea, kwa mujibu wa TMZ.
Mnamo mwaka wa 2023, #AbeDiaw aliwasilisha kesi ya madai dhidi ya mwimbaji huyo, akimtuhumu kumpiga kwa chupa ya tequila kwenye Club cha usiku jijini London. Hata hivyo, Ijumaa iliyopita, #Diaw anaripotiwa kuwasilisha nyaraka kwa jaji wa Kaunti ya L.A. akiomba kesi hiyo ifutwe.
Maombi hayo yanaonesha kuwa #Diaw anataka kesi ifutwe kwa moja kwa moja (with prejudice), hali ambayo inazuia kesi hiyo kufunguliwa tena siku za usoni. Mara nyingi aina hii ya kufuta kesi hutokana na makubaliano ya kifedha, ingawa bado haijathibitishwa kama kulikuwa na makubaliano yoyote ya malipo.
Iwapo jaji ataidhinisha kufutwa kwa kesi hiyo, Brown bado atakabiliwa na kesi yake ya jinai inayoendelea kuhusiana na tukio hilo hilo. Mapema mwaka huu, alikamatwa alipoingia Uingereza kwa ajili ya ziara yake ya kimataifa na kufunguliwa mashtaka ya shambulio pamoja na umiliki wa silaha na waendesha mashtaka wa nchini humo.