Rais Samia Kuhusu Kupungua kwa Mfumuko wa Bei kwenye Kipindi Chake

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

20 hours ago
rickmedia: rais-samia-kuhusu-kupungua-kwa-mfumuko-bei-kwenye-kipindi-chake-633-rickmedia

Rais Samia Suluhu Hassan Akihutubia na Kuhitimisha Shughuli za Bunge la 12 la la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania June 27.2025 katika ukumbi wa Bunge Aligusia swala la Kupungua kwa Mfumuko wa Bei kwenye kipindi chake.

Katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa katika kudhibiti mfumuko wa bei. Takwimu zinaonesha kuwa mfumuko wa bei umepungua kutoka wastani wa asilimia 5.6 mwaka 2020 hadi asilimia 3.0 mwaka 2025, na hivyo kufikia kiwango cha tarakimu moja (single digit), jambo ambalo linaonesha uthabiti wa sera za uchumi na usimamizi mzuri wa fedha za umma.

Kupungua huku kwa mfumuko wa bei kumeleta ahueni kwa wananchi wengi, hususan katika gharama za maisha. Mfano halisi ni kupungua kwa bei ya bidhaa muhimu ya chakula kama sukari, ambapo bei yake kwa wastani sokoni imeshuka kutoka TZS 3,000 kwa kilo mwaka 2020 hadi TZS 2,717 kwa kilo mwaka 2025. Hili ni ishara ya kupungua kwa shinikizo la bei kwa bidhaa za msingi, na hivyo kuimarisha uwezo wa wananchi kununua mahitaji yao ya kila siku.