Loading...

Wabunge wa Afrika Kusini kuanza kupiga Kura za kumchagua Rais

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: wabunge-afrika-kusini-kuanza-kupiga-kura-kumchagua-rais-539-rickmedia

Wabunge kutoka Vyama 18 vya Siasa wanapiga Kura leo Juni 14, 2024 kumchagua Rais wa Taifa hilo ikiwa ni takriban wiki 2 tangu kumalizika kwa Uchaguzi wa Wabunge

Rais Cyril .Ramaphosa kutoka Chama Kikongwe cha African National Congress (ANC) anawania kurejea tena kuongoza licha ya Chama chake kudaiwa kuendelea kupoteza ushawishi.

ANC yenye Wabunge 159 kati ya 400, inakabiliwa na upinzani mkali kutoka Chama cha Democratic Alliance (DA) chenye Wabunge 87, idadi ambayo imeilazimu ANC kukubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Jaji Mkuu ataongoza shughuli za uapisho wa Wabunge ili waruhusiwe kupiga Kura. Kwa mujibu wa Katiba, inatakiwa robo tatu ya Wabunge wote wawepo Bungeni ili Uchaguzi ufanyike