Kesi Ya Diddy Inaelekea Ukingoni, Mashahidi Hawatoruhiswa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: kesi-diddy-inaelekea-ukingoni-mashahidi-hawatoruhiswa-48-rickmedia

Kesi ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono dhidi ya #Diddy inaonekana kufikia ukingoni bila shahidi hata mmoja kutoa ushahidi kwa niaba ya utetezi wake.

Kwa mujibu wa CNN, waendesha mashtaka wanapanga kuhitimisha kesi yao dhidi ya msanii huyo mashuhuri wa muziki wa hip-hop mwenye umri wa miaka 55. Shahidi wa mwisho wa upande wa mashtaka, wakala maalum Joseph Cerciello kutoka Idara ya Upelelezi wa Usalama wa Ndani (Homeland Security Investigations), anatarajiwa kukamilisha ushahidi wake, jambo litakalohitimisha uwasilishaji wa upande wa mashtaka.

Timu ya mawakili wa utetezi wa #Diddy imeiambia mahakama kuwa hawatatoa mashahidi wowote hata Combs mwenyewe hatatoa ushahidi.

Kwa mujibu wa CNN, mawakili wake watatoa ushahidi mdogo tu kabla ya kuanza kwa hoja za mwisho za kesi.