CRDB wamedai Pesa za Mshindi wa FA msimu uliopita (YANGA SC) wameshatoa muda kwa TFF.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: crdb-wamedai-pesa-mshindi-msimu-uliopita-yanga-sc-wameshatoa-muda-kwa-tff-454-rickmedia

Benki ya CRDB na Wadhamini Wakuu wa Kombe la Shirikisho Tanzania Wametoa barua kujibu tuhuma za Klabu ya Yanga Sc kupitia Afiisa Habari wa Klabu hiyo Ally Kamwe kuwa hawajalipwa Pesa za Ushindi wa Msimu uliopita wa 2024/25 na hawatoshiriki Fainali za mashindano hayo Msimu huu mpaka walapwe.

Barua ya CRDB imesema kuwa tayari Pesa hizo zimeshatolewa kwa TFF Muda mrefu.

"Benki ya CRDB inapenda kutoa ufanunuzi wa madai yaliyotolewa na Msemaji wa Klabu ya Yanga katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika tarehe 09 Juni 2025 katika Makao Makuu ya klabu hiyo.

Katika mkutano huo, Msemaji wa Klabu hiyo alinukuliwa akitoa taarifa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kwetu kama Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB kuwa Klabu ya Yanga haitocheza fainali za mashindano hayo msimu huu kama hawatolipwa fedha za ubingwa wa msimu uliopita.

Tungependa kuufahamisha umma na wadau wote wa soka kuwa Benki ya CRDB ni taasisi yenye kuzingatia weledi, kanuni na taratibu na kwa msingi huo tayari Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF.

Benki ya CRDB inatambua kuwa mbali na mchezo wa soka kuunganisha jamii yetu na kutoa burudani, lakini pia mchezo huu ni ajira kwa vijana wengi, hivyo dhamira yetu ni kuendelea kushirikiana na TFF, vilabu na wadau wengine katika kukuza mchezo huu kwa maslahi mapana ya Taifa letu."