Mwanzilishi mwenza wa jukwaa la kutuma ujumbe la #Telegram amesema anagawanya utajiri wake kwa watoto wake na anasema ana angalau watoto 106.
#PavelDurov, mwenye umri wa miaka 40, aliiambia #LePoint, chombo cha habari cha Ufaransa, katika mahojiano kuhusu uamuzi wake wa kugawa mali zake, Kwa mujibu wa jarida la Forbes, anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 17.1.
#Durov, ambaye ana watoto sita waliopatikana kwa njia ya kawaida ya uzazi, alisema pia amekuwa mtoaji wa mbegu za kiume kwa wanawake ambapo amesema ana watoto zaidi ya 100 katika nchi 12.
“Nataka kufafanua kwamba sifanyi ubaguzi kati ya watoto wangu: Kuna wale waliotungwa kwa njia ya kawaida na wale waliotokana na mchango wangu wa mbegu,” alisema. “Wote ni watoto wangu na wote watakuwa na haki sawa!”
#Durov alisema watoto wake hawatapata urithi wao hadi miaka 30 kupita tangu siku aliyotoa mahojiano hayo kwa Le Point, ambayo ni Juni 19, mwaka 2055.
“Nataka waishi kama watu wa kawaida, wajijenge wenyewe, wajifunze kujitegemea, waweze kuunda vitu, wasitegemee akaunti ya benki,” alisema.
Durov aliamua kugawa urithi wake mapema kwa sababu ya matatizo ya kisheria yanayoikumba Telegram, Programu hiyo ya kutuma ujumbe, iliyoanzishwa mwaka 2013, ni maarufu kwa huduma zake za faragha Lakini jambo hilo pia limeleta changamoto na migogoro na vyombo vya sheria.
Mamlaka za Ufaransa zilimshtaki Pavel mwezi Agosti 2024 na kumtuhumu kuwa mshirika katika kuendesha jukwaa linalohusiana na shughuli haramu — kama vile usambazaji wa maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto, biashara ya dawa za kulevya, na udanganyifu.