Muigizaji wa filamu #DerekDixon amemshutumu Muigizaji na mwandishi wa filamu #TylerPerry kwa unyanyasaji wa kingono, akidai kwenye kesi kwamba mfanyabiashara huyo mashuhuri alifanya juhudi za mara kwa mara za kumtongoza na alijaribu kuficha tukio la unyanyasaji kwa kumpa fursa ya kuingiza kwenye Filamu yake.
Malalamiko hayo yenye kurasa 46, yaliyowasilishwa wiki iliyopita katika Mahakama Kuu ya Kaunti ya Los Angeles, yanadai fidia ya jumla ya dola milioni 260 kama adhabu, na yanalinganisha madai hayo na yale dhidi ya watu wengine mashuhuri wa tasnia ya burudani waliowahi kushutumiwa kwa makosa ya kingono.
Katika taarifa, wakili wa Perry alimtuhumu mlalamikaji, Derek Dixon, kwa kujaribu kumkaribia Perry kwa kile kinachoonekana kuwa mpango wa kutapeli. Wakili huyo alisema:
“Lakini Tyler hatakubali kutishwa kwa njia hii na tuna uhakika madai haya ya kubuni ya unyanyasaji hayatafaulu.”
Kulingana na kesi hiyo, Perry alimtumia Dixon ambaye wakati huo alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya matukio nafasi yake ya kwanza ya kuigiza mwaka 2019.
Miezi michache baadaye, alimkaribisha Dixon nyumbani kwake huko Georgia na akampatia vinywaji kadhaa kabla ya kumwambia alale katika chumba cha wageni, kulingana na mashtaka hayo.
Perry anadaiwa kupanda ghafla kitandani kwa Dixon na kuanza kumshika shika , kwa mujibu wa hati hiyo ya mashtaka.