Zumaridi akamatwa na Polisi kwa kuwaambia watoto yeye ndio Mungu wao

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: zumaridi-akamatwa-polisi-kwa-kuwaambia-watoto-yeye-ndio-mungu-wao-261-rickmedia

Jeshi la Polisi limemkamata na linamhoji Diana Edward Bundala “Mfalme Zumaridi” (42), Mkazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa kwa tuhuma tofauti ikiwemo kuwaeleza Watoto yeye ni Mungu wao mwenye uwezo wa kuwatenganisha na kifo.

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali.

Pia, Jeshi la Polisi limewaomba Wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi.