Dkt.Janabi kuiwakilisha Tanzania, uchaguzi wa Mkurugenzi wa WHO- Afrika

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: dktjanabi-kuiwakilisha-tanzania-uchaguzi-mkurugenzi-who-afrika-150-rickmedia

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa na Mshauri wa Rais Masuala ya Afya, Profesa Yakub Janabi, ametangazwa rasmi kuiwakilisha Tanzania katika Uchaguzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, baada ya Mkurugenzi Mteule wa nafasi hiyo Dkt. Faustine Ndugulile, kufariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Janabi ni miongoni mwa Wagombea Watano na uchaguzi utafanyika Geneva Mei 18, 2025.

Aidha, Dkt. Janabi ni Mgombea pekee kutoka nchi za Kusini mwa Janga la Sahara, huku wagombea wengine wakitokea Ivory Coast, Guinea, Niger na Togo.