Mahakama ya rufaa nchini Mauritania imemhukumu Rais mstaafu, Mohamed Abdel Aziz kifungo cha miaka 15 jela na faini ya dola milioni 3 baada ya kukata rufaa kupinga kifungo cha miaka mitano.
Aziz alihukumiwa mwaka wa 2023 kwa utakatishaji fedha ambapo akiwa madarakani, alijipatia mali yenye thamani ya Dola milioni 70 [TZS bilioni 188.8].