Ligi Kuu: Simba Pointi 69, Yanga Pointi 70

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: ligi-kuu-simba-pointi-69-yanga-pointi-365-rickmedia

Magoli yaliyofungwa na Steven Mukwala yameiwezesha Timu ya Simba kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya KMCFC ambayo imepata goli kupitia kwa Rashid Chambo katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa KMC.

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 69 ikiwa nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi nyuma ya Yanga yenye pointi 70, timu zote hizo mbili zikiwa zimecheza michezo 26.

Upande wa KMC imesalia katika nafasi ya 11 ikiwa na alama 30 katika michezo 27.