Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Joseph Nyamoko na Issa Masoud wamefariki Dunia baada ya kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama.
Taarifa ya Jambo TV imeeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amesema tukio hilo limetokea katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro na kuwa mipango ya kusafirisha miili ya askari hao inaendelea kwa uratibu wa Jeshi la Polisi na Familia za wahusika.
Aidha, Nyamoko na Issa kila mmoja ameacha Mke na watoto wawili.