Son afungua kesi dhidi ya mwanamke aliyesema ana ujauzito wake

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 hours ago
rickmedia: son-afungua-kesi-dhidi-mwanamke-aliyesema-ana-ujauzito-wake-399-rickmedia

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min (32) amefungua kesi Polisi dhidi ya Mwanamke ambaye alidai ana ujauzito wa staa wake akidai kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kupata fedha.

Wanasheria wa Son wanadai Mdada huyo alitoa madai hayo Juni 2024 na akataka fedha ili anyamaze, wiki iliyopita Son akaamua kufungua mshtaka kwa kuamini mtu huyo alikuwa na lengo la kumlaghai ili ajipatie fedha.

Son hana mke wala Mtoto anayetambulika na aliwahi kunukuliwa akisema “Baba alisema unapooa kipaumbele cha kwanza ni familia, mke na Watoto kisha soka. Nataka kuhakikisha nitaendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu, nikistaafu ndio nitaanza kutafuta Watoto.”