Muuzaji wa Barakoa #BonifaceKariuki ambae alipigwa risasi kichwani na polisi wakati wa maandamano ya jana Nchini Kenya , yupo hai, familia yake imethibitisha; baba yake, #JohnNyamburaKariuki, amesema risasi ilipita kichwani, juu kidogo ya sikio.
Mbali na hivyo Familia imesema kuwa Taarifa zinazozagaa mitandao kuwa mtoto wao amepoteza maisha sio Za kweli na wanamuombea arudi kwenye hali yake.
Maafisa wawili wa Polisi , #MasindeBarasa na #DuncanKiprono, waliorekodiwa kwenye camera wakimpiga risasi mfanyabiashara ndogondogo, #BonifaceKariuki, jijini Nairobi,Kenya wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
Ripoti za awali zinaonyesha kuwa mhanga alipigwa risasi ya mpira, ambayo ilisababisha majeraha sehemu ya juu ya mwili wake, hasa kichwani.