Ali Kamwe:Bodi ya Ligi ikiridhia matakwa ya Yanga,tutacheza Derby ya Kariakoo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: ali-kamwebodi-ligi-ikiridhia-matakwa-yangatutacheza-derby-kariakoo-517-rickmedia

 Wakati Uongozi wa #Yanga ukitarajiwa kufanya kikao na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, leo Juni 9, 2025 kuhusu ajenda ya mchezo dhidi ya #Simba uliopangwa kuchezwa Juni 15, 2025, Klabu hiyo imesema matakwa yao yakisililizwa na kutekelezwa, timu itaingia uwanjani.

Akijibu swali kupitia Wasafi FM, Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema “Yanga ni Klabu ya Mpira wa Miguu, kazi kubwa ni kucheza Mpira wa Miguu, matakwa ya Kamati ya Utendaji ya Yanga yaliyowasilishwa kwa Bodi ya Ligi yakisikilizwa na yakafanyiwa kazi bila shaka yoyote mbungi itapigwa.”

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Machi 8, 2025 lakini uliahirishwa baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa siku moja kabla, Yanga ilipeleka timu uwanjani na kueleza haipo tayari kucheza mchezo huo Namba 184 wakati mwingine kwa madai maamuzi ya kutochezwa yalikuwa kinyume na utaratibu wa Kanuni za Ligi.