Mzazi Mwenzie na 50 CENT adai 50 ni Mnyanyasaji Alimpiga Akiwa Mjamzito

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

8 hours ago
rickmedia: mzazi-mwenzie-cent-adai-mnyanyasaji-alimpiga-akiwa-mjamzito-644-rickmedia

Mwanamke Aliezaa Mtoto wa Kwanza wa 50 cent #ShaniquaTompkins alidai kuwa baba wa mtoto wake, rapa #50Cent, alimshambulia kimwili alipokuwa na ujauzito wa mtoto wao, #MarquiseJackson, Pia alidai kuwa alimshambulia mama wa mtoto wake wa pili, #DaphneJoy na kudai ndio sababu ya kuamua kuachana nae.

Akiwa Live kwenye ukurasa wake wa Instagram Alisema kuwa #50Cent Ni Mnyanyasaji na katili mpaka leo.

“Alinipiga nikiwa ujauzito wa Marquise. Tumbo lilikuwa kubwa tayari.”

“Kwa sababu alikuwa mkatili. Yaani bado ni mkatili. Kihisia, kimwili.“

Tompkins pia alieleza kwa nini alichagua kutohusika katika kesi ya Joy, akidai kuwa hakuwa na uhusiano mzuri na Joy kutokana na mambo aliyosema kumhusu. “Mimi ni mama kwanza na pia ni mwanamke, lakini katika kipindi cha uhusiano kati yake na 50, alinipiga vijembe sana na alinishambulia mtandaoni pamoja naye. Kama kwamba alijiona bora na alifikiri yeye na mtoto wake walikuwa bora kuliko Marquise na mimi,” alisema Tompkins.

Mapema mwezi huu, shahidi aliyejitambulisha kwa jina la bandia Jane Doe alitoa ushahidi katika kesi ya Diddy, na rapa wa wimbo “Many Men” akauliza hadharani kama mlalamikaji huyo alikuwa ni Daphne Joy. Mnamo Juni 6, Fif aliposti picha ya Joy na mchoro wa mahakamani akiwa ameandika: “Hey kuna yeyote anajua Jane Doe ni nani? Najaribu kufanya utafiti kwa ajili ya documentary ya Diddy,” akafuatisha na emoji ya macho wazi. Chapisho hilo tangu wakati huo limefutwa.