Iran Yalipua Hospital Ya Israel, Wamwaga Machozi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: iran-yalipua-hospital-israel-wamwaga-machozi-520-rickmedia

Majeshi ya Iran yametupa makombola mbalimbali kwenye Ardhi ya Israel na kujeruhi makumi ya watu.

Moja kati ya sehemu iliyoathirika na mashambulizi hayo ni pamoja na Hospitali ya Soroka Hospital ambapo kwa mujibu wa Iran inadai kuwa ilishambulia eneo hilo ikilenga uongozi na Makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) karibu na hospitali.

 Israel yatoa kauli baada ya Iran kuishambulia moja kati ya Hospital nchini humo mapema leo

Waziri wa Afya wa Israel Uriel Buso amesema kuwa Iran imevuka mstari kwa kushambulia Hospitali na kukiita kitendo hicho kama "Kosa la Jinai la Kivita".

Hata hivyo kwa upande wa Iran wamesema kuwa walishambulia eneo hilo kwakuwa lipo karibu na makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF)