Watu 11 wamefariki dunia kwenye Kiwanda kinachohusika na uzalishaji wa Sukari nchini Tanzania Mtibwa Sugar baada ya kutokea kwa hitilafu ya Mitambo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema kuwa "Tukio limetokea saa 7:30 usiku kuamkia leo Mei 23,2024, kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme"
"Waliofariki ni wataalam wa umeme na mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo "SACP Alex amesema kuwa kati ya waliofariki kuna Raia watatatu wa Kigeni kutoka Kenya, Brazil na India ambapo miili ya wote waliopoteza maisha imehifadhiwa kwenye Hoispitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiendelea kupatiwa matibabu kwenye katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala