Ben Pol Afunguka Mipango Ya Kuacha Muziki

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

5 hours ago
rickmedia: ben-pol-afunguka-mipango-kuacha-muziki-145-rickmedia

Msanii wa Muziki wa R&B Ben Pol Amefunguka kuhusu mipango ya kuacha Muziki na kusema kuwa kama siku itatokea Ataacha Muziki hatotangaza kwa namna yoyote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ameandika..

"Japo sijafikiria na sina mpango huo kabisa! lakini ikitokea siku nikaamua kuacha kufanya Muziki hakutakuwa na tangazo, wala waraka…kama ambavyo miaka kadhaa nyuma watu walishtukia tu kuna mtu anaitwa Ben Pol anaimba, vivyo hivyo watashtukia kuna mtu alikuwa anaitwa Ben Pol ila siku hizi haimbi.

Moyoni nitakuwa na amani kwamba nimehudumu vizuri kwa nyimbo, maisha yangu na jumbe villivyogusa maisha ya watu na ku-inspire, kwa sababu ni Kweli,

na hilo nikijua mimi itakuwa imetosha, mengineyo yatakuwa ni ziada 🙏🏼

Binafsi siamini sana kwenye “Legacy” naona ni mambo ya kutaka kujipa umuhimu hata ukishaenda,

Naona ni kitu kilianzishwa zamani na Mtawala, Mfalme au Mtu mwenye nguvu ambaye hakuwa humble.. wazo lake lilikuwa kwamba hata akienda aendelee kuheshimiwa, kusujudiwa au kutajwa kwa yale aliyoyafanya,

Sidhani kama ina tija!

Maisha ya binadamu yameanza zaidi ya miaka 200,000 iliyopita, kweli kabisa tukukumbuke?! Sasa tutakumbuka watu wangapi?

Au kwamba miaka 200,000+ ijayo wanadamu wa wakati huo watukumbuke sisi wa sasa?, ni kazi ngumu sana kuwapa waja katikati ya mambo yote yanayoendelea Duniani; Climate change, Umasikini, Kukosekana kwa usawa wa Vipato, Afya, Chakula na Maji , Haki za Binadamu, Silaha za Nyuklia, AI n.k

Kila nikiangalia Mtoto wangu wa miaka 9 hamjui @roma_zimbabwe ndo naishiwa nguvu kabisaa 🤣

Sikia, hudumia kwa nguvu na moyo wako wote kwa kutumia kipawa chako, ujuzi, taaluma, karama yako…

Na tunakupenda ila TUTAKUSAHAU 🤩🤝❤️

Nawatakia uhudumu mwema, tenda wema nenda zako.

Acha alama hata kama Itafutika."

Ben Pol alianza rasmi safari yake ya muziki aliapokuwa sekondari. Alianza kuimba shuleni na kujiunga na Tanzania House of Talents (THT) alipokuwa sekondari, miaka ya mapema ya 2007–2008.

Baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2010, Duke Tachez alimchagua chini ya studio za M‑Lab (Music Laboratory) huko Dar es Salaam, ambapo alipewa mkataba wa kurekodi na kufanya albamu yake ya kwanza “Maboma” ambayo ilitoka Februari 2011