Rais Wa China Asema Dunia Bila Marekani Inawezekana

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

5 hours ago
rickmedia: rais-china-asema-dunia-bila-marekani-inawezekana-913-rickmedia

Rais wa China Xi Jinping ameripotiwa kutoa ujumbe mzito kwa Marekani, akisisitiza kuwa dunia ina uwezo wa kuendelea bila uongozi wa taifa hilo. Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya Marekani katika uongozi wa dunia na mwelekeo wa nguvu za kimataifa.

Katika hotuba yake iliyojawa na mafumbo ya kihistoria, Xi Jinping alitolea mfano wa tawala zilizowahi kutawala dunia kama vile Uingereza, Ufaransa, na Hispania ambazo hatimaye ziliporomoka baada ya kupoteza ushawishi wao wa kimataifa. Kwa mujibu wa wachambuzi, ujumbe huo ulikuwa ni dokezo kuwa Marekani nayo inaweza kukumbwa na hatma kama hiyo iwapo haitalinda heshima na ushawishi wake wa kimataifa.