Suala la kuacha urithi ni wajibu wa wazazi hata kwenye vitabu vya dini vimeandika juu ya hili, lakini kwa muigizaji mkongwe Jackie Chan kwake mambo yapo tofauti sana Chan hataki kabisa kumuachia mali za urithi mtoto wake wa kiume Jaycee.
Staa huyo mwenye utajiri wa zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 400 ameweka wazi kuwa watoto wake wanapaswa kutafuta pesa zao wenyewe na kuacha kutegemea mali zake za urithi.
Chan amenyooshea kidole kabisa mtoto wake wa kiume Jaycee kuwa hatopata mali za urithi kutoka kwake. Chan anasema kuwa "Mwanangu anauwezo wa kupata pesa zake mwenyewe, kama hana uwezo wa kutafuta zakwake basi anauwezo wa kupoteza zakwangu.
Mwaka 2015 Jackie alizua maswali mengi kwa mashabiki mara baada ya kulipia tiketi yake ya Ndege daraja la hadhi ya juu kisha mtoto wake kumkatia darahja la kawaida jambo ambalo lilishangaza watu wengi sana