P.Diddy ashtakiwa tena kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: pdiddy-ashtakiwa-tena-kwa-kesi-unyanyasaji-kingono-76-rickmedia

Rapa Diddy Ameingia Kwenye Msala Tena. Ni Muendelezo Wa Kesi Zake Za Unyanyasaji Wa Kijinsia, Ambapo Kwa Sasa Ameshtakiwa Kwa Unyanyasaji Wa Kingono dhidi ya Aliyekuwa Producer Wake Rodney Jones Jr, akidai kufanyiwa ukatili huo pamoja kudhulumiwa malipo ya uandaaji Albamu ya ‘The Love Album: Off the Grid’.

Katika madai yake, Jones anasema kati ya mwaka 2022 na 2023, alikuwa akiishi nyumbani kwa Diddy ambapo alishikwa maumbile yake, kutakiwa kufanya vitendo vya ngono na Wanawake wanaojiuza, kushiriki mapenzi ya jinsia moja, pia kulazimishwa kutumia Dawa za Kulevya na Pombe

Jones anaongeza kuwa Diddy alimshinikiza kufanya hivyo huku akimuahidi atampa Tuzo, kumfanya awe maarufu pamoja na kumtafutia kazi kwenye kampuni kubwa za biashara za Muziki. Jones anamtaka Diddy amlipe fidia ya Dola za Marekani Milioni 30 (takriban Tsh. BILIONI 76,500,000,000).

Hata Hivyo Wanasheria Wa Diddy Wameibuka Na Kukanusha madai hayo na kueleza kuwa Jones ametunga kashfa hizo kwa lengo la kujipatia Fedha