Balozi wa Tanzania Vatican mwenye Makazi Berlin, Ujerumani, Hassani Iddi Mwamweta, amewasilisha salamu za pongezi na kheri kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Baba Mtakatifu Leo wa XIV.
Kwenye salamu hizo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Papa leo XIV kufuatia kuchaguliwa kuwa Papa wa 267 na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani. Aidha, amemuahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Kwa upande wake Papa Leo XIV ameeleza kuwa amefurahi kupokea salamu kutoka Tanzania, nchi ambayo anaipenda kwa kuwa ameshawahi kuitembelea mara kadhaa akiwa anatekeleza majukumu ya kikazi na ameelezea utayari wake kufanya kazi kwa karibu na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika.
Salamu hizo zimewasilishwa baada ya Sherehe ya Kusimikwa rasmi kama Rais wa Vatican na Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, sherehe hizo zimefanyika kwenye Basilica la Mt. Petro, Vatican.