Maafisa wa Upelelezi wa Polisi wa Metropolitan wamemkamata mwimbaji #ChrisBrown, mwenye umri wa miaka 36, saa nane usiku katika Hoteli ya The Lowry mjini Manchester, Uingereza, baada ya kugundua kuwa alikuwa amewasili jijini humo kwa ndege ya kibinafsi saa chache kabla.
#Brown amekamatwa kwa tuhuma za kusababisha madhara makubwa ya mwili kwa mtayarishaji wa muziki Abe Diaw katika klabu ya usiku ya Tape iliyoko Mayfair, katikati mwa London, mwezi Februari 2023.
Amewekwa kizuizini na inadhaniwa kuwa alipelekwa hadi kituo cha polisi cha karibu kwa ajili ya kuhojiwa.