Davido amjibu anayedai kuwa ni binti yake "Tumefanya DNA Test 5"

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: davido-amjibu-anayedai-kuwa-binti-yake-tumefanya-dna-test-533-rickmedia

Davido ameweka wazi msimamo wake kufuatia ombi la kipimo cha DNA kutoka kwa binti anayejitambulisha kama mtoto wake, akisisitiza kuwa suala hilo tayari limeshafanyiwa uchunguzi wa kutosha.

Kupitia ukurasa wake wa X, Davido amesema kuwa walikubaliana kuchagua hospitali kwa pande zote mbili, ambapo yeye alichagua hospitali tatu huku upande wa pili ukichagua hospitali mbili, na matokeo ya vipimo vyote yalionyesha kuwa hana uhusiano wa damu na mtoto huyo.

“Vipimo vyote vilitoka negative. Hii ndiyo mara ya mwisho nitaongea kuhusu upuuzi huu,” aliandika Davido.

Msanii huyo aliongeza kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano na mama wa mtoto huyo, akisema walikutana tu wakati wa taratibu za vipimo vya DNA. Aidha, alieleza masikitiko yake juu ya jinsi suala hilo lilivyoendelea, akisisitiza kuwa hamlaumu mtoto, bali anaona mzazi ndiye aliyechangia kuendeleza madai hayo.

Kauli hizo zimeibua mjadala mpana mitandaoni, huku baadhi ya watu wakimuunga mkono Davido kwa kusimamia ukweli wa matokeo ya kitabibu, na wengine wakieleza masikitiko yao kwa mtoto anayehusika, wakisisitiza umuhimu wa kulinda afya ya akili ya watoto katika migogoro ya aina hiyo.

Davido amehitimisha kwa kusema anataka suala hilo lifikie tamati na asihusishwe tena na madai hayo.