Jaji Atupilia mbali Kesi ya R kelly dhidi ya TashaK

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

19 hours ago
rickmedia: jaji-atupilia-mbali-kesi-kelly-dhidi-tashak-722-rickmedia

Jaji mmoja wa Illinois ametupilia mbali kesi ya #RKelly dhidi ya #TashaK kufuatia kushindwa kuendeleza mashtaka.

Katika malalamiko yaliyowasilishwa Novemba 2023 katika mahakama ya shirikisho mjini Chicago, mawakili wa #Kelly walidai kuwa afisa wa Idara ya Magereza (BOP) aliingilia kwa njia isiyo halali kumbukumbu za kidijitali za gerezani za #Kelly.

Kumbukumbu hizo zilijumuisha rekodi za mazungumzo ya simu ya faragha kati yake na mpenzi wake pamoja na mawakili wake.

Inadaiwa kuwa afisa huyo aliwauzia Tasha rekodi hizo, na baadaye Tasha kuzirusha kwenye jukwaa lake. Hata hivyo, jaji alitupilia mbali kesi hiyo baada ya timu ya Kelly kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha kuendeleza mashtaka.