Daktari maarufu wa Plastic Surgery mjini Beverly Hills, #RonaldMoy, amefariki dunia kutokana na matatizo yaliyojitokeza baada ya kufanyiwa Upasuaji wa Shingo, Amefariki Akiwa na umri wa miaka 68.
Ronald Moy, daktari mashuhuri wa upasuaji katika kikundi cha Moy, Fincher, Chipps Facial Plastics and Dermatology kilichopo North Rodeo Drive huko Beverly Hills, alifariki dunia tarehe 23 Juni akiwa hospitalini kutokana na “matatizo ya upasuaji wa shingo,” kulingana na tovuti ya Mchunguzi wa Vifo wa Kaunti ya Los Angeles.
Moy alikuwa na taaluma ya juu, akiwa amewahi kuwa rais wa American Academy of Dermatology, American Society of Dermatologic Surgeons, na American Board of Facial Cosmetic Surgery. Pia alikuwa profesa katika Shule ya Tiba ya David Geffen katika Chuo Kikuu cha UCLA.
Mbali na mbinu za kawaida za upasuaji wa uso na plastiki, Moy alikuwa mtaalamu wa upasuaji wa Mohs micrographic, ambao ni mchakato makini na wa hatua kwa hatua wa kutibu vidonda vya saratani ya ngozi, kulingana na Johns Hopkins Medicine.
Mpaka Kufikia wakati wa kifo chake, Moy alikuwa amefanya zaidi ya upasuaji 30,000.