Ahukumiwa Miaka Minne kwa Kula Pesa Za Kanisa Milioni 983

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

10 hours ago
rickmedia: ahukumiwa-miaka-minne-kwa-kula-pesa-kanisa-milioni-983-563-rickmedia

Mzee Terence Capstick (75) wa Winslow, Buckinghamshire, amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kukutwa na hatia ya wizi wa £285,000 kutoka Kanisa la Winslow Parish na taasisi ya misaada ya Rogers Free Educational Trust kati ya Januari 2019 na Oktoba 2023. 

Alichukua £163,600 kutoka akaunti ya kanisa na £122,052 kutoka kwenye taasisi hiyo, akitumia vibaya nafasi yake ya mhasibu wa kujitolea. 

Alikamatwa Machi 19, 2024 na kufikishwa mahakamani ambapo alikiri mashtaka mawili ya udanganyifu kwa kutumia nafasi ya kuaminika.