Whozu Afunguka Mazito Kudhulumiwa na Lebo yake ya Zamani

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

6 hours ago
rickmedia: whozu-afunguka-mazito-kudhulumiwa-lebo-yake-zamani-70-rickmedia

Staa wa Muziki #Whozu ameishtumu Kampuni ya #Empire kwa Kushikilia Akaunti zake (YouTube) licha ya kuacha kufanya nao kazi baada ya kujiunga Tangu 2023.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Whozu Ameandika 

“Dhulma: Ona Watu wasivyokua na huruma na jasho la mtu. Account yangu ya Youtube haiko sawa, jinsi inavyosoma views na inavyo display ni vitu viwili tofauti..

Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu hali yangu na kampuni ya

Empire Music Distribution. Tangu nijiunge nao mwaka 2023, Nilishindwa kufanya nao kazi Nikajitoa kwao. Lakini stil Mpaka leo hawajanirudishia Account yangu ya youtube

Na hawajatoa MCN Yao kwenye account, ( Multi channel

Network) Na sipewi ushirikiano Wowote, kujibiwa Emails zangu, sio simu, Wamenikalia tu kimya na bado promotion ya nyimbo zangu nafanya kwa pesa yangu mwenyewe..

Aidha, mtu aliyehusika mimi kujiunga na kampuni hii, ambae nimfanya kazi wao anae tambulika kwa jina Alma, @almah_bronxi amekosa ushirikiano kabisa, na hii baada

ya kusema najitoa kwenye kampuni yao..

Ninaomba viongozi wakuu wa Empire Music Distribution kunisaidia hili kwa haraka:

1.

Kunitoa kwenye mfumo wao wa usambazaji wa

muziki.

2. Kunipa malipo yote yanayostahiliwa kwa kazi

zangu zilizokusanywa kipindi chote nilichokuwa

nikishirikiana nao.”