Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia askari wanne wa Jeshi Usu kwa tuhuma za kumuua kijana Eziboni Fikiri (20) wa Kijiji cha Msonga, Bukombe, Agosti 13, 2025 katika Pori la Hifadhi ya Kigosi.
Inadaiwa walikuwa wakiwakamata watu waliokata miti kinyume cha sheria. Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe na uchunguzi ukiendelea kabla ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani.