Gari La Mgombea Udiwani Lachomwa Moto

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: gari-mgombea-udiwani-lachomwa-moto-594-rickmedia

Katika mchakato wa kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM), gari la mgombea udiwani wa Kata ya Igwachanya, Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Anthony Mawata, limechomwa moto na watu wasiojulikana alfajiri ya Agosti 4, 2025.

Kwa mujibu wa Mawata, tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri karibu na nyumbani kwake, ambapo gari lilikuwa limeegeshwa gereji. Alidai kuwa alikuta gari limeungua huku vijana waliokuwa na mapanga wakiwa jirani na eneo hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo na wahusika.

Tukio hili linajiri wakati kura za maoni za CCM zikiendelea nchini huku maeneo mengine yakiripoti utulivu, vurugu na vituko mbalimbali.