Mahakama Kuu imeamuru mashahidi wa kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, #TunduLissu walindwe kwa siri.
Mashahidi hao, ambao ni raia, watatoa ushahidi bila kuonekana, majina yao hayatatamkwa wala taarifa zozote zitakazowatambulisha wao au watu wa karibu nao.
Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 4, 2025, na Jaji Hussein Mtembwa kufuatia maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Aidha, vyombo vya habari vimezuiwa kusambaza taarifa hizo bila ruhusa ya Mahakama.
Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 huko Mbinga na kufikishwa mahakamani Dar es Salaam Aprili 10, 2025.