Kituo cha Habari cha #CNN Kilizungumza na wakili wa #Diddy na wakaambiwa kuwa timu yake imewasiliana na utawala wa #Trump kuomba msamaha wa rais.
Kituo hicho cha habari kiliripoti kuwa Ikulu ya White House ilijibu ombi lao la kutoa maoni kwa kusema kuwa hawatatoa maoni kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ombi lolote la msamaha.
Ikumbukwe kwenye moja ya mahojiano ya Rais #Trump Alisema hatatoa msamaha wa rais kwa Rapa huyo licha ya historia yao ya urafiki wa karibu.
Trump Alieleza kuwa uhusiano wao ulivunjika kutokana na kile alichokitaja kuwa ni tabia ya dharau aliyofanyiwa na Diddy wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa urais.