Atupwa Jela kwa kuandika mtandaoni "Bora Rais asingezaliwa"

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: atupwa-jela-kwa-kuandika-mtandaoni-bora-rais-asingezaliwa-287-rickmedia

Muuguzi mmoja aitwaye Tokpa Japhet mwenye umri wa miaka 43 ametupwa jela kwa kile kilichoelezwa andiko lake la Facebook aliloandika; 'Bara la Afrika lingenusurika endapo Rais Alassane Outtara hangezaliwa".

Kutokana na kauli hiyo Japhet kutoka nchini Ivory Coast ametupwa jela miaka mitatu wakati ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya taifa hilo kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali, Oumar Kone katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu Julai 21,2025, amesema Japhet amehukumiwa kifungo hicho na kupigwa faini ya dola 8,500 licha ya kuomba msamaha.

Imeelezwa muuguzi huyo alienda mbali zaidi na kuandika "Mama yake Ouattara angetoa mimba angeokoa Afrika".

Tovuti ya TRT na Arab News zimeeleza Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema mashtaka hayo ni sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na utovu wa nidhamu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo linaongezeka mara kwa mara.

Katika hatua nyingine Rais Ouattara (83), hajathibitisha iwapo atawania muhula wa nne, ingawa amependekezwa na chama chake kufanya hivyo.