Msanii maarufu wa muziki wa hip hop na muigizaji, Busta Rhymes, anatarajiwa kupewa heshima kubwa ya kupatiwa nyota ya Hollywood Walk of Fame mnamo Agosti 1, 2025, katika hafla maalum itakayofanyika katika jiji la Los Angeles, Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Biashara cha Hollywood (Hollywood Chamber of Commerce), Busta Rhymes atakuwa miongoni mwa watu mashuhuri wachache wanaopewa nyota kwa kutambua mchango wao mkubwa katika sekta ya burudani, hasa kupitia muziki wa hip hop.
Nyota hiyo itakuwa ya 2,818 katika orodha ya nyota za Hollywood Walk of Fame