Ozzy Osbourne Afariki Dunia Akiwa na Miaka 76

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: ozzy-osbourne-afariki-dunia-akiwa-miaka-311-rickmedia

Gwiji wa muziki wa rock, Ozzy Osbourne, amefariki dunia akiwa na umri wa Miaka 76.

Kifo chake kimetokea wiki chache tu baada ya nyota huyo wa Black Sabbath kupanda jukwaani kwa mara ya mwisho akiwa pamoja na wenzake wa bendi katika uwanja wa Villa Park, Birmingham.

Familia yake imetangaza kifo chake Jioni ya Julai 22.

Ozzy, aliyefahamika kama Mwana wa Giza kutokana na matendo yake ya kisanii jukwaani yaliyomvutia maelfu ya mashabiki wa muziki wa heavy rock, alitumbuiza nyimbo tano kwa mara ya mwisho mwezi huu, akiwa amerejea jukwaani na wenzake Geezer Butler, Tony Iommi na Bill Ward.