Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM, SACP Muliro Jumanne, amesema si kila wakati askari anaweza kujitambulisha au kueleza kosa la mtuhumiwa wakati wa kumkamata, hasa kama mtuhumiwa ana silaha au anakimbia.
Amesema sheria inataka askari ajitambulishe na kueleza kosa, lakini mazingira halisi wakati mwingine hayaruhusu.
Ametoa wito kwa jamii kuelewa kuwa ustaarabu unahitajika kutoka pande zote mbili askari na mtuhumiwa.
"Nashangaa watu wanasema askari hajajitambulisha anapokwenda kumkamata mhalifu. Inategemea na mazingira kama mhalifu ana silaha?
"Au alipomuona askari anakimbia! Atajitambulisha vipi? Au wanasema askari hajamwambia mhalifu kosa lake.
Atamwambiaje wakati yeye ni mkata mapanga?
"Hajamaliza kumwambia kosa lake si atakuwa ameshamkata mkono? Wakati mwingine askari anaanza kujitambulisha mhalifu anafoka na hampi nafasi askari ya
kujitambulisha anafika kituoni anasema hajaambiwa kosa
lake”.