Carlo Ancelotti Ahukumiwa Mwaka Mmoja Jela

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: carlo-ancelotti-ahukumiwa-mwaka-mmoja-jela-401-rickmedia

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil na aliyewahi kuwa meneja wa Real Madrid na Chelsea, #CarloAncelotti, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai wa kodi unaohusiana na kipindi chake akiwa Real Madrid mwaka 2014.

Mamlaka za Uhispania zilimtuhumu #Ancelotti, mwenye umri wa miaka 66, kwa kushindwa kutangaza mapato kutokana na haki za picha, hali iliyosababisha ukwepaji wa kodi wa zaidi ya pauni 833,000. Ingawa Ancelotti alikanusha kufanya makosa kwa makusudi, alikiri kulipa kodi pungufu mwaka huo, akieleza kuwa ni kosa la kihasibu.

Aliondolewa mashtaka mengine yaliyohusiana na mapato yake ya mwaka 2015. Licha ya hukumu hiyo ya hatia, #Ancelotti hatarajiwi kutumikia kifungo hicho gerezani, kwani sheria za Uhispania huruhusu wafungwa wa mara ya kwanza ambao si wakatili na waliopatikana na hatia ya kifungo kisichozidi miaka miwili, kutotumikia kifungo jela.

Ancelotti aliifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2013 na 2015 kabla ya kuhamia Bayern Munich.