Katika tukio la kusikitisha daktari mmoja kutoka Mumbai, India ameripotiwa kupotea baada ya kudaiwa kujirusha kutoka kwenye daraja la Atal Setu.
Daktari huyo mwenye umri wa miaka 32, Dr. Omkar Bhagwan Kavitake, ambaye alikuwa akifanya kazi katika Hospitali ya JJ, ameripotiwa kupotea baada ya kuruka kutoka kwenye daraja hilo usiku wa Jumanne.
Inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo, Dr. Omkar alimpigia simu mama yake na kumwambia kuwa alikuwa anarudi nyumbani kwa ajili ya chakula cha jioni.
Dereva mmoja aliyekuwa akipita kwenye daraja la baharini la Atal Setu ambalo ndilo daraja refu zaidi la baharini nchini India na linaunganisha Mumbai Kusini na Navi Mumbai -aliona mtu akipanda reli ya daraja na kuruka. Shahidi huyo aliwataarifu polisi haraka.