Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kurejesha adhabu ya kifo kwa mtu yeyote atakayefanya mauaji katika mji mkuu Washington D.C. Lengo la hatua hiyo ni kupunguza wimbi la uhalifu jijini humo.
Trump amesema: “Ikiwa mtu ataua mtu katika mji mkuu — Washington D.C. tutatoa hukumu ya kifo Hatuna chaguo.”
Ikumbukwe kuwa mwaka 1981, D.C. ilifuta adhabu ya kifo, lakini sasa Trump ameirudisha tena. Wananchi wengi wameonyesha kufurahishwa na uamuzi huo wakiamini kwamba unawalenga watuhumiwa wanaohusika na makosa makubwa