Jose Chameleone Afunguka Kukubali Ombi la Talaka

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

8 hours ago
rickmedia: jose-chameleone-afunguka-kukubali-ombi-talaka-449-rickmedia

Nguli wa muziki nchini Uganda, Joseph Mayanja “Jose Chameleone”, amezungumzia mchakato wa talaka yake na mkewe Daniella Atim baada ya ndoa ya miaka 17. Chameleone amesema amekubali mali zigawanywe lakini hakubaliani na kulazimishwa kusaini wosia akiwa bado hai. Ametoa msimamo kuwa mali wanazogombea ni za watoto wao watano, si mali binafsi. Mkewe alifungua kesi ya talaka Machi na Agosti 21 Mahakama ilikubali, kutokana na madai ya kutelekezwa na kutopendwa. Chameleone amesisitiza hana pingamizi kwa hatua za kisheria na amewahakikishia mashabiki kuwa anaendelea kuwa na amani licha ya mvutano huo.