Watu 158 Wamefariki kwa Kipindupindu Sudan

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: watu-158-wamefariki-kwa-kipindupindu-sudan-2-rickmedia

Takriban watu 158 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika eneo la Darfur, Sudan. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya jimbo hilo linalodhibitiwa na wanamgambo wa RSF, vifo hivyo vimeripotiwa kuanzia mwishoni mwa Mei 2025.

Mamlaka za afya zimesema hali hiyo inachochewa na ukosefu wa maji safi, dawa na huduma za afya, huku mapigano yanayoendelea yakizidisha ugumu wa kupatikana kwa misaada ya dharura.

Mashirika ya kimataifa yameonya kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi.